Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANESCO yashauri ukarabati vifaa viwandani

TANESC TANESCO yashauri ukarabati vifaa viwandani

Fri, 10 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHIRIKA la Umeme (TANESCO), limewataka wamiliki wa viwanda kufanya ukarabati wa mara kwa mara wa vifaa vilivyotumika kwa muda mrefu, ili kuondokana na matumizi makubwa ya umeme.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mhandisi Mtafiti wa Shirika hilo, Aurea Bigirwamungu, alipokuwa akitoa elimu ya matumizi bora ya nishati ya umeme katika Wilaya za Bahi na Dodoma.

Alisema wamiliki hao wanatakiwa kuwa na utamaduni wa kufanya ukarabati huo ili kujiepusha na gharama zisizo za lazima na matumizi hayo makubwa.

“Wamiliki wanatakiwa kuwa na utamaduni wa kubadilisha mota za kuendeshea mitambo yao katika uzalishaji ili kutumia nishati ya umeme inayoendana na gharama ya matumizi sahihi ya nishati ya umeme kwenye viwanda vyao,” alisema.

Kwa upande wake, Ofisa Tawala wa Kampuni ya Nyanza Road Workers, Bakari Mugini, alishukuru kwa kupatiwa elimu hiyo ambayo imesaidia kujua matumizi ya umeme kwa kampuni.

“Tumepata elimu juu ya usalama wa miundombinu iliyopo viwandani ili kuongeza uzalishaji katika kampuni zao,” alisema.

Alisema elimu iliyotolewa na shirika hilo itasaidia kutoa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha umeme mkoani Dodoma unakuwa wa uhakika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live