Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANAPA waongezewa fedha uratibu Hifadhi za Taifa

Pesa Fedhaddd TANAPA waongezewa fedha uratibu Hifadhi za Taifa

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Mheshimiwa Naibu Spika, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) linasimamia hifadhi za Taifa 22 zenye ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 104,578 kwa sasa, wakati za mwanzo zilikuwa 16 ambazo zilikuwa na kilometa za mraba 57,107.

Kuongezeka kwa idadi ya Hifadhi zinazoongozwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kutoka hifadhi 16 hadi hifadhi 22, kumepelekea kuwa na changamoto ya fedha za uendeshaji na za kutekeleza miradi ya uwekezaji ya hifadhi, kutokutekeleza miradi ya uwekezaji ya hifadhi kunaathiri upatikanaji wa mapato ya kutosha kutokana na kupungua kwa watalii kwani mazingira ya hifadhi hayarithishi, hivyo kukosekana ufanisi na tija ya uwekezaji katika hifadhi,

Bunge linaazimia kwamba, Serikali ihakikishe inaipatia Shirika la TANAPA fedha za kutosha ili kuongeza ufanisi katika hifadhi zote 22 hivyo, waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu na tija iweze kupatikana.” Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Umma (PIC) kwa kipindi cha kuanzia Februari 2022 hadi Januari, 2023, Jerry Silaa (Mb).


Chanzo: www.tanzaniaweb.live