Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAEC yawafunda wanaokagua mizigo kwa mionzi mahotelini

Ec00e8d372fc9071037cfab4ccd19fcd TAEC yawafunda wanaokagua mizigo kwa mionzi mahotelini

Fri, 5 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAFANYAKAZI wa kukagua mizigo na bidhaa mbali mbali za wageni wa ndani na nje kwa kutumia mionzi, wamefanya mafuzo hayo kwa vitendo katika maeneo ya viwanja vya ndege, maabara za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) na katika hoteli jijini Arusha.

Mratibu wa mafunzo hayo kutoka TAEC, Atumaini Makoba amesema mafunzo kwa vitendo yanasaidia maeneo ambayo mionzi inapotoka haswa kwenye mashine za ukaguzi wa mizigo ili waweze kupunguza wigo wa mionzi wanayopata pasipo lazima wakati wa kufanya kazi zao.

“Hapa sasa tunawaonesha yale waliyosoma darasani kwa vitendo ili kuwapa ujuzi zaidi kwani itawasaidia kuepukana na madhara ya mionzi maana lazima anayepima mizigo afahamu kwa kina wapi mionzi inapotokea na inapoelekea wakati akifanya kazi hiyo,”alisema Makoba.

Amesema katika kujifunza kwa vitendo ameona wapo baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakikosea katika utendaji wao wa kila siku, lakini baada ya kuwaonesha kwa vitendo wameweza kurekebisha pale walipokuwa wakifanya tofauti.

Kwa upande wake kiongozi wa maofisa hao waliohudhuria mafunzo kwa vitendo, Lusajo Masosi amesema mafunzo hayo ya vitendo yamewejengea uwezo wa namna ya kujilinda na athari za mionzi katika maeneo yao ya kazi.

Jumla ya maofisa 40 kutoka katika maeneo ya ujenzi wa miundombinu kama barabara na mamlaka mbalimbali kama vile viwanja vya ndege, hotelini, viwandani na bandarini wanashiriki mafunzo hayo ya matumizi salama ya teknolojia ya mionzi kwa siku tano makao makuu ya TAEC-Arusha.

Chanzo: habarileo.co.tz