Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAA yawasilisha tozo ya huduma za usalama viwanja vya ndege

17543 TAA+PIC TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imetoa taarifa kwa waendeshaji wa mashirika ya ndege za abiria zinazofanya safari zake kuanzia e kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) juu ya tozo ya huduma za usalama wa viwanja vya ndege, ambayo haikuwepo awali.

Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela amesema utekelezaji wa tozo hiyo ambayo ni dola tano kwa abiria wa nje ya nchi na Sh5,000 kwa abiria wa ndani, utaanza rasmi Oktoba Mosi, 2018.

Akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu kaimu mkurugenzi wa fedha na biashara wa TAA, Pius Wankali amesema agizo la ukusanywaji wa tozo hiyo ulitangazwa na Mamlaka ya Usafiri wa  Anga (TCAA) Juni, 2018.

“Tangazo la kuanzishwa kwa tozo hii lilichapishwa na TCAA kutoka kwenye nyaraka AIC Doc No. TCAA/FRM/ANS/AIS-30, Juni 29 2018 na utekelezaji wake utakuwa kuanzia Oktoba Mosi, 2018," amesema Wankali.

Mwakilishi wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL), Ismail Ismail alitaka kuwepo kwa maelezo ya kina juu ya tozo hiyo, ambayo alitaka ijumuishwe ndani ya tiketi ili abiria awe ameilipia moja kwa moja.

Mwakilishi wa Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM), Alexander Van de Wint ameomba tozo hiyo  ianze baadaye mwakani kutokana na wao tayari wameshauza tiketi za hadi Desemba 2018.

Chanzo: mwananchi.co.tz