Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAA yakabidhiwa Uwanja wa Ndege KIA

Kilimanjaro Airport Terminal Building TAA yakabidhiwa Uwanja wa Ndege KIA

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dar es Salaam. Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) imekabidhi rasmi Kiwanja cha Ndege cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA).

Taarifa iliyotolewa leo Novemba 11 na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Uchukuzi ilisema uwanja huo umekabidhiwa jana mkoani Kilimanjaro.

Hatua hiyo imekuja kufuatia tamko la Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alilolitoa Novemba 9 bungeni Dodoma kufuatia mvutano uliodumu kwa mwaka mzima, huku wabunge wakitaka TAA ichukue majukumu ya Kadco.

Akizungumza leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya uwanja huo Waziri wa Uchukuzi, Profesa Mbarawa amesema pamoja na mabadiliko hayo yaliyofanyika, Serikali itazingatia stahiki zote za Wafanyakazi zinalipwa kulingana na sheria.

“Kiwanja cha KIA ni kiwanja cha kimkakati pamoja hivyo pamoja mabadiliko yaliyofanyika tayari kuna kikosi kazi kinatakachohakikishwa Viwango vya uendeshaji vinaendelea kukua na maslahi ya watumishi yanapatikana kulingana na Sheria za utumishi zilizopo,” amenukuliwa Profesa Mbarawa.

Waziri Mbarawa amesema kuwa mabadiliko ya uendeshaji yaliyofanywa yanakwenda sanjari na maboresho katika usafiri wa anga yanayojikita katika ununuzi wa ndege mpya na ujenzi wa viwanja vya ndege ili kurahisisha shughuli za kibiashashara ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso amesema ni wakati sasa wa Serikali kuhakikisha miradi ya ujenzi wa viwanja vya ndege ambayo iko chini ya Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) na TAA inasimamiwa kwa karibu ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyarara amewahakikishia wadau wote kuwa pamoja na mabadiliko hayo huduma zitaendelea kutolewa kwa kuzingatia miongozo na kanuni za kimataifa zinazooognoza usafiri wa anga.

Taarifa hiyo imesema Kadco ni kampuni iliyosajiliwa Machi 11, 1998 kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni, Sura ya 212.

“Julai 6, 1998 Serikali iliamua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) uendeshwe kupitia sekta binafsi ambayo ilikuwa kwa njia ya ubia kati yake na kampuni ya Mott MacDonald ya Uingerereza, South African Infrastructure Fund ya Afrika Kusini na Kampuni ya InterConsult ya Tanzania,” imesema taarifa hiyo.

Imeongeza kuwa ubia huo uliingia kwa mikataba miwili ambayo ni Mkataba wa Uendeshaji (Concession Agreement) pamoja na Mkataba wa Ukodishaji (Lease Agreement) baina yake na KADCO.

Taarifa hiyo imesema kutokana na uendeshaji usioridhisha wa uwanja huo, mwaka 2010 Serikali iliamua kununua hisa za wanahisa wenza wa Kadco kwa kuvunja mkataba wawanahisa na hivyo Kadco kumilikiwa na Serikali asilimia 100.

“Iliendelea kuendesha KIA ikiwa ni kampuni ya Serikali kupitia Mikataba ya Uendeshaji (Concession Agreement) na Ukodishaji (Lease Agreement) ambayo ukomo wake ambao umefikia mwisho Novemba 9, 2023 na Novemba 9, 2023, Serikali imeamua kuhamisha shughuli za Uendeshaji kutoka KADCO kwenda TAA.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live