Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Super Feo alianza na mtaji wa elfu 20

Super Feo UWF Super Feo

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara na mwekezaji Maarufu nchini Tanzania kutokea mkoani Ruvuma, Omary Marcus Msigwa unaweza kumuita Super Feo, amesimulia historia yake ya kibiashara na kusema alianza biashara akiwa na mtaji wa fedha isiyozidi Shilingi Elfu 20 za kitanzania miaka 30 iliyopita.

Super Feo amesema hayo wakati alipotembelewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kiwandani kwake ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani.

Bilionea huyo ambaye kwa sasa anamiliki shule, kiwanda cha unga, mabasi na malori ya kusafirishia makaa ya mawe amewataka wajasiriamali kutoogopa kuanza biashara kwa kutumia mtaji mdogo walionao.

"Mimi hapa nikikwambia muda ninaoamka na muda ninaolala ni vitu tofauti. Mimi kila siku naamka saa 11:00 asubuhi lakini nalala saa 7:00 ya usiku kila siku. Haya ndio maisha yangu. Sasa mtu mwingine hawezi kuamini lakini ndio ukweli. Muda mwingi nautumia kwenye kufanya kazi".

"Tatizo sio mtaji, kinachotakiwa ni nidhamu ya kazi. Watanzania wengi wakati mwingine nidhamu ndio tatizo. Mtaji unaweza kuupata kutokana na nidhamu yako, hata kama umeajiriwa, unaweza ku-save pesa yako kidogokidogo na ukaweza kuanza maisha yako," ameongeza.

Wewe unasubiri uwe na shilingi ngapi ndio uanze Biashara?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live