Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sumatra yaonya kuhusu kupandisha nauli

31821 Mwanzapic TanzaniaWeb

Sat, 15 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Uongozi wa mkoa umefanikiwa kudhibiti tabia wamiliki wa mabasi ya mikoani kutokupandisha nauli kiholela wakati huu wa kuelekea Sikukuu.

Ofisa mfawidhi  wa Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri wa Nchi Kavu (Sumatra), mkoani Mwanza, Gabriel Anthony amesema hatua kali zitachukuliwa kwa wote watakaoenda kinyume na taratibu ikiwemo kufutiwa leseni.

Amesema mamlaka hiyo imekuwa ikiendesha kampeni maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wananchi kuhusiana na namna ya kutambua nauli halali ya kutoka mji hadi mji kwa kutumia simu zao za mkononi, tangu Agosti 2018 hadi Jumatatu 2018.

“Elimu ambayo tumekuwa tukiitoa ni pamoja na jinsi ya kuijua nauli na haijalishi aina ya simu. Simu yeyote tu ina uwezo wa kupata majibu ya nauli,” amesema Anthony.

Amefafanua kwamba, abiria kabla hajaenda kukata tiketi, anatakiwa kuingia kwenye simu yake, upande wa jumbe aandike neno Nauli aache nafasi, sehemu alipo, nafasi na anapokwenda kisha aitume kwenye namba 15200, ujumbe huo unagharimu Sh150/- tu na atapata majibu ndani ya dakika mbili baada ya kutuma.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz