Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Suma JKT kulinda ofisi za mali za TTCL nchi nzima

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa TTCL Waziri W. Kindamba. TTCL

Thu, 7 Jun 2018 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeingia mkataba wa mwaka mmoja wa ulinzi wa majengo, mali na miundombinu yake na Kampuni ya Suma JKT.

Mkataba huo umeanza kutekelezwa Juni Mosi baada ya makubaliano yote muhimu kukamilika baina ya watendaji wa pande zote mbili. Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema wanajisikia faraja kushirikiana na kampuni hiyo inayomilikiwa na jeshi kwani wana imani watafanya kazi yao kwa weledi.

“Awali tuliwapatia kazi ya ulinzi makao makuu ya shirika na Kituo cha Kimataifa cha Kutunzia Kumbukumbu (NIDC) kilichopo Kijitonyama. Wamefanya kazi yao kwa weledi, nidhamu na ufanisi mkubwa ndiyo maana tumeamua kuwakabidhi jukumu la kulinda ofisi zetu nchi nzima,” alisema Kindamba.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa JKT, Kanali Aristides Rutta alisema licha ya nidhamu na ujuzi wa kijeshi walio nao vijana wake, kampuni hiyo inajivunia mafunzo na vifaa vya kisasa vya kazi, rekodi iliyotukuka katika utekelezaji wa miradi ya wananchi na nyenzo za ulinzi na usalama walizonazo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live