Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Suluhu ya Amcos kuuza kahawa kimagendo yapatikana

Kahawa Pc Suluhu ya Amcos kuuza kahawa kimagendo yapatikana

Sat, 6 May 2023 Chanzo: Mwananchi

Wadau wa kahawa mkoani Kagera wamependekeza Vyama vya Ushirika vya Msingi (Amcos) 14 vilivyopo maeneo ya mipakani kupewa fedha mapema ili zisiuze zao hilo kimagendo.

Wadau wa kahawa mkoani Kagera wamependekeza Vyama vya Ushirika vya Msingi (Amcos) 14 vilivyopo maeneo ya mipakani kupewa fedha mapema ili zisiuze zao hilo kimagendo. Wadau hao wamepitisha mapendekezo hayo Mei 05, 2023 katika mkutano wao uliofanyika mjini Bukoba. Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa nchini (TCB), Primus Kimalio amesema amcos hizo zinapaswa kuuza kahawa tani 3, 000 hadi 4, 000 kwa msimu lakini zimekuwa zikiuza tani 1, 000 jambo linaloonyesha kahawa nyingine inauzwa kwa Amesema ili kuondoa tatizo hilo, zitafunga mkataba mapema na vyama vya ushirika au wanunuzi binafsi wa kahawa kwa ajili ya kuinunua huku TCB ikihusika kupanga bei kulingana na bei ya mnada kwa wakati huo. “Katika kuondoa tatizo la wakulima waliopo mpakani kuuza kahawa kwa njia ya magendo amcos hizi zitapewa fedha mapema kwa kufunga mkataba na vyama vya ushirika au wanunuzi binafsi ili kahawa hiyo inunuliwe hapa nchini na mapato yarudi kunufaisha watanzania” Amesema Kimalio Awali akifungua mkutano huo, Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa hotuba yake kwa kujiuliza maswali na kujijibu ambapo alianza kujiuliza ni kwa namna gani amcos zilizopo mpakani zimeweza kufikisha kahawa kwenye mnada? je hawalimi kahawa au wana mifumo yao ya kuiuza? Mkuu huyo wa mkoa amejijibu kwa kusema ni kwa sababu amcos hizo hazina fedha tasilimu ya kununua kahawa ya mkulima na kuuliza namna gani zinaweza kusaidiwa na kama hakuna mikataba inayoweza kufungwa na vyama hivyo. Baada ya mjadala mrefu, yakatolewa mapendekezo mbalimbali likiwemo la amcos hizo kupewa fedha mapema ili mkulima asiweze kuwa na mawazo ya kuuza kahawa ya magendo. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, James John amesema iwapo wakulima hao watapata fedha mapema itawaondolea kuuza kahawa yao kwa njia ya magendo na amcos zitanufaika na Sh70 wanayopata kwa kila kilo huku vyama vya ushirika vikipata Sh30.

Chanzo: Mwananchi