Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sukari ya Zanzibar yazua gumzo jipya Bungeni

5907 Bunge TZW

Fri, 6 Apr 2018 Chanzo: mtanzania.co.tz

Mbunge wa Chambani, Yusufu Salum Hussein (CUF), amesema kero za Muungano zimeanza karne zilizopita, lakini hazijawahi kutatuliwa.

Aidha, amesema hivi karibuni mawaziri wa biashara na viwanda wa Zanzibar na Bara walikutana kutatua changamoto ya suakari lakini wakashindwa.

“Zanzibar kuna tani 460,000 za sukari lakini Serikali ya Muungano imeikataa na inaenda kunua Brazil na kisingizo cha kukataa ni kwa maelezo kuwa Zanzibar watanunua sukari nje wakachanganye na yao kisha kuuza bara,” amesema.

Kutokana na hilo, amesema lengo la kutatua kero za muungano hazipo.

Kwa upande wake Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Kessy, alimkatisha kwa kutoa taarifa akisema sukari inayozalishwa Zanzibar haitoshi kwa matumizi ya Wazanzibar sasa iweje watake Tanzania bara inunue.

“Mnataka sisi tuwe jalala la wafanyabiashara wa Zanzibar kwa sukari za magendo,” amesema.

Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji, alimpa taarifa Hussein akasema; “Kiwanda cha Zanzibar kina uwezo wa kuzalisha tani 8,000 za sukari kwa mwaka wakati mahitaji ya Zanzibar ni tani 17,000 mpaka tani 20,000, kwa hiyo msemaji ajielekeze kwenye hoja asipotoshe wananchi.”

Hata hivyo, Hussein alikataa taarifa hiyo kwa maelezo kuwa waziri anajua mambo ya fedha na siyo biashara kwasababu kinachotakiwa kuangaliwa ni bei ya soko na siyo sukari inatoka wapi.

Hata hivyo, mabishano hayo yalizua mjadala mwingine baada ya Mbunge wa Konde, Khatibu Said Haji, kusema kitendo cha Naibu Waziri wa Fedha kusema sukari ya Zanzibar haitoshelezi Zanzibar hivyo haiwezi kuletwa Bara, ni kumdhalilisha Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akikaa vikao kushughulikia suala hilo.

“Mnachofanya ni kumdhalilisha Makamu wa Rais, kwanini mnamuacha ajadili jambo ambalo mnajua haliwezekani, ni aibu kwenu wote,” amesema Haji.

Amesema Zanzibar hakuna kiwanda cha bia lakini zinatoka bara na kwenda kwenye visiwa hivyo, lakini anashangaa sukari inayozalishwa huko kuzuiwa kuingia bara.

 

Chanzo: mtanzania.co.tz