Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Subash aomba uwezeshaji matumizi ya gesi kwenye viwanda

20876 Viwanda+pic TanzaniaWeb

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imeshauriwa kufikiria upya kutumia gesi ili kufufua viwanda na kuongeza mwamko kwa wawekezaji, kufungua viwanda vipya kwani umeme ni unasuasua.

Akizungumza leo Oktoba 4,2018 katika Jukwaa la Fikra la Mwananchi linalolenga kujadili fursa, changamoto na ufumbuzi kuelekea uchumi wa viwanda ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Subash Patel amesema Tanzania ni nchi yenye vyanzo vingi vya uzalishaji wa umeme na gesi.

Amesema ingawa gesi inazalishwa nchini haijatoa mrejesho mzuri kama nchi.

“Gesi yetu imekaa, umeme wetu ni wa kusuasua mimi nina kiwanda, (lakini) bado tunatumia makaa (ya mawe) na yanaleta madhara, hiyo gesi hatujaweka katika uchumi wa viwanda kikamilifu,” amesema Patel.

Patel ambaye amekuwa mchokoza mada katika jukwaa hilo amegusia madini kwamba hayajaongezwa thamani kikamilifu.

“Kwa mfano chumvi asilimia 50 tunaagiza kutoka nje. Tujiulize kwa nini watu hawawekezi. Usumbufu wanaoupata, tukifanya hivyo tutakaribisha uwekezaji kutoka nje kwa ukubwa.

“Tanzania ina bahari inakuja Vox Wagon (kampuni ya magari) wanapeleka kiwanda Rwanda. Tujiulize kwa nini tumekosa mwekezaji kama huyo?” amehoji.

Waziri Mwijage hawezi kuzuia bidhaa kuuzwa nje ya nchi

Chanzo: mwananchi.co.tz