Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stendi ya Mwenge yakamilika tayari kwa kuanza kazi!

Stand Mwenge .jpeg Stendi ya Mwenge yakamilika tayari kwa kuanza kazi!

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Stendi mpya ya Mwenge imekamilika kwa 100% na itaanza kufanya kazi rasmi baada ya taratibu nyingine zikiwemo za upangishaji wa fremu kukamilika.

Ujenzi umegharimu Tsh. bilioni 10.067 na fedha hizo zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Kinondoni na Mkandarasi aliyejenga ni Heinan International LTD kutoka China.

Kwa mujibu wa taarifa ya Viongozi wa Halmashauri ya Kinondoni, fremu zote za biashara katika stendi hii zimepangishwa kupitia mnada ambao ulifanyika kwa mfumo wa TAUSI TAMISEMI kuanzia October 18-26, 2023 kwa njia ya mtandao.

Stendi ina uwezo wa kuchukua mabasi 100, bajaji 20 na pikipiki 40 kwa mara moja na ina vibanda vya kupumzikia abiria 27.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live