Stendi ya mabasi ya Magufuli iliyopo Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam, imekusanya Sh bilioni 3.4 katika kipindi cha miezi 10 cha mwaka wa fedha 2021-22, zinazotumika kuimarisha miundombinu mbalimbali ya huduma kwenye stendi hiyo.
Hayo yamebainishwa na Ofisa Habari wa Manispaa ya Ubungo, Joina Nzali jana, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mwezi mmoja kwa wananchi kuhusiana ulipaji ushuru, ada, tozo na kodi mbalimbali zinazotozwa na halmashauri hiyo, kampeni iliyoanza jana na inatarajia kukamilika Juni 6 mwaka huu.
Joina alibainisha, lengo la mwaka wa fedha wa 2021/22 unaoishia mwezi ujao ni kukusanya Sh bilioni 23 na tayari imekusanya Sh bilioni 18, huku akisisitiza kuwa maofisa kodi wa Ubungo wameongeza ubunifu katika kusimamia kodi na tozo nyingine, ili kuhakikisha makusanyo yanapatikana kwa ufanisi.
Amesema msisitizo wa kukusanya mapato katika Stendi ya Magufuli umefanikisha kupatikana kiasi hicho cha fedha, kinachotumiwa kuhudumia abiria na wananchi wanaopata huduma katika stendi hiyo na kuimarisha miundombinu kadhaa mfano ujenzi wa daraja linalounganisha stendi hiyo na Kituo cha Mabasi ya Mbezi mwisho