Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Standard Chartered yaisaidia Red Cross, UNICEF bil. 1.2/-

Standard Chartered Standard Chartered yaisaidia Red Cross, UNICEF bil. 1.2/-

Fri, 10 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BENKI ya Standard Chartered Tanzania imetoa Sh. bilioni 1.2 kwa Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross) Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali ikiwamo elimu na afya.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sanjay Rughani, alisema katika taarifa kuwa kati ya dola 550,000 zilizotolewa na benki (sawa na shilingi bilioni 1.265) kati dola 300,000 zimegawiwa kwa Red Cross na dola 250,000 kwa UNICEF.

“Benki ya Standard Chartered inajivunia kuchangia fedha kwa ajili ya mipango mbalimbali ya Red Cross Tanzania na UNICEF, hivyo kusaidia makundi yaliyo katika mazingira hatarishi,” alisema Sanjay.

Alisema benki imekuwa ikifadhili shughuli mbalimbali za kusaidia wananchi hasa katika mabara ya Asia na Afrika kama ya afya, mawasiliano, miradi ya elimu ili kuzisaidia nchi za mabara hayo.

Alisema Red Cross ambayo inafanya kazi maeneo mbalimbali duniani, itasaidia kutolewa kwa huduma za afya katika shule za msingi na sekondari maeneo mbalimbali duniani, mawasiliano, kutoa mavazi maalum ya kujikinga na maradhi hasa kwa wataalamu wa afya wa kujitolea na waajiriwa pamoja na kutoa huduma ya chakula kwa waathirika wa virusi vya corona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live