Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Soko lilivyofunga kiwanda cha chaki

Chaki Za Maswa Soko lilivyofunga kiwanda cha chaki

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

KIWANDA cha chaki cha Victoria kinachomilikiwa na kampuni ya Arwa Investment kilichopo wilayani Tarime, Mkoa wa Mara kilichozinduliwa na aliyekuwa Makamu wa Rais (sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), Samia Suluhu Hassan, kimefungwa baada ya kukosa soko la kuuza chaki mkoani humo.

Imeelezwa kuwa licha ya mkoa wa Mara kuwa na shule nyingi za msingi na sekondari na vyuo, lakini hazinunui chaki zinazozalishwa na kiwanda hicho badala yake zinazonunuliwa ni za kutoka mikoa mingine na nchi jirani ya Kenya.

Meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Magala Magembe, alisema kuwa kitendo cha bidhaa za ndani kutonunuliwa kunarudisha nyuma jitihada za wawekezaji wa ndani kwa kuwa watu wengi hawapendi kununua bidhaa za kwao na kukimbilia zile za nje.

"Kiwanda kilianza uzalishaji 2017, tuna miezi sita sasa kiwanda kimesimama uzalishaji kwa sababu chaki hazinunuliwi.

Chanzo: ippmedia.com