Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Soko la parachichi layoyoma, vita ya Ukraine na Russia yatajwa

Kilimo Cha Parachichi Scaled Hali ya hatari yatangazwa soko la parachichi nchini

Sat, 16 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima na wasafirishaji wa zao la parachichi wamelalamika kuporomoka kwa soko la zao hilo na kueleza sababu kubwa ni kukosekana kwa meli za kusafirisha shehena za mizigo kulikosababishwa na vita kati ya Russia na Ukraine.

Meneja Rasirimali watu wa Kampuni ya Kuza Afrika inayojihusisha na kilimo na usafirishaji wa shehena za parachichi katika nchi za India, Dubai na Russia, Noel Kabuje amesema hayo leo Ijumaa Aprili 15, 2022 baada ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk Vincent Anney kutembelea vituo vya ukusanyaji na kuona hali halisi ya upatikanaji wa zao hilo pamoja na taarifa ya masoko ya ndani na nje ya nchi.

''Mkuu wa Wilaya changamoto ni nyingi lakini  vita ya Russia imechochea sana kuporomoka kwa soko la parachichi kutokana na utegemezi mkubwa wa kutumia meli  ambazo asilimia kubwa zinamilikiwa na raia wa nchi hiyo ambapo baada ya kuibuka mapigano  zimesitisha safari. Kwa sasa tunakwama namna ya uendeshaji ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa masoko ya kusambaza shehena za mzigo uliopo''amesema.

Kabuje amesema kwa sasa wanasafirisha wastani wa tani 40 sawa na kontena mbili hadi moja za zao hilo tofauti na awali walikuwa wakisafirisha tani 100 ambayo ni sawa na kontena tano.

Mkulima na Mjumbe wa bodi ya Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Parachichi wilaya ya Rungwe  (Uwamaru), Christopher  Mwene amesema hali hiyo imechochea kundi kubwa la madalali kununua parachichi kwa Sh600 kwa kilo badala ya bei elekezi ya Serikali ya Sh1,600.

Naye, Mkuu wa Wilaya, Dk Vicent Anney amesema amefikia hatua ya kukagua vituo vya manunuzi ya ya zao hilo baada ya kuwepo kwa taarifa zinazodaiwa matunda hayo kuozea shambani kutokana na kukosekana kwa masoko.

Advertisement  ''Kimsingi sijafurahishwa kwa kauli ambazo zinazunguka kuwa matunda yanaozea shambani nimefika na kujiridhisha. Kuna wanunuzi wanaendelea kuingia shambani licha ya kuwepo kwa changamoto ya soko  ''amesema

Dk Anney amesema kutokana na changamoto hiyo, Serikali  itaona namna ya kupata masoko ya ndani ikiwa ni pamoja na kudhibiti madalali wa kati wanaoingia kuwarubuni wakulima na kununua zao hilo kwa kilo Sh600 badala ya bei elekezi ya Serikali Sh 1,600.

Amesema katika kuthibiti hilo pia wataweka utaratibu mzuri kwa kila kijiji kuwa na kikundi ambacho wakulima watakuwa wakikusanya parachichi linaloingizwa sokoni na kwenda kuuza kwa utaratibu maalum na kwamba mfumo wa kuuza kiholela imekuwa mwiba kwa wakulima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live