Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Soko la mazao ya bahari lazinduliwa Kikungwi Zanzibar

Soko La Mazao Ya Bahari Lazinduliwa Kikungwi Zanzibar Soko la mazao ya bahari lazinduliwa Kikungwi Zanzibar

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amewataka wajasiriamali wa Soko la Chaza Kikungwi kudumisha usafi ili liwe endelevu na kivutio kwa Watalii.

Akizungumza katika uzinduzi wa Soko la mazao ya baharini, huko Kikungwi Wilaya ya Kati, ikiwa ni shamrashamra ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema Watalii wanaoingia nchini wanapenda mazao ya Baarini ikiwemo Chaza hivyo ni vyema kudumisha usafi katika maeneo yao.

"Usafi ni muhimu na biashara ya Chaza inapendwa na wageni wa kitalii,” alisema Waziri.

Aidha amewataka kufuata utaratibu wa wafanyabiashara wa chakula kwa kupima Afya zao na kuvaa nguo maluum zinazotakiwa.

Akisoma taarifa ya kitaalamu, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Malum za SMZ Issa Mahfoudhi Haji alisema ujenzi wa Soko hilo itapelekea kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao.

Nae Katibu wa kikundi Cha kuuza Chaza Kikungwi Bahati Issa Suleiman alisema kuwepo kwa Soko hilo kumewapa faraja kwani ni Soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao sambamba na kuahidi kulienzi na kulitunza ili liweze kuwa endelevu.

Soko hilo limejengwa na kampuni ya Mzawa Modarn Building Contractor LTD, umegharimu zaidi ya milioni 300 ambapo ujenzi wake ulianza tarehe 23/3/2023 na umekamilika rasmi 25/11/2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live