Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Soko la bidhaa za asili lazinduliwa Dar

Soko la bidhaa za asili lazinduliwa Dar

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Soko la bidhaa za asili na mazao yanayotoka shambani limezinduliwa katika soko la wakulima Oysterbay.

Soko hilo lililoanzishwa mwaka 2013 linafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) chini ya mradi wa Boresha Lishe.

Akizungumza kabla ya kukabidhi soko hilo linalosimamiwa na EU kwa kushirikiana na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na shirika lisilo la serikali ya Italy (CEFA), mkuu wa ushirikiano wa umoja huo, Jose Correia Numes amesema soko hilo linauza bidhaa kutoka vijiji mbalimbali nchini.

"Watu wanaweza kununua bidhaa za asili ambazo zinapatikana hapo na sio katika masoko mengine, " amesema.

Amesema zaidi ya wachuuzi 30 hufungua maduka kwenye soko hilo kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ambako vyakula vya asili, matunda, mboga, mayai, kahawa hupatikana.

Amebainisha kuwa wachuuzi wanaouza bidhaa kwenye soko hilo ni wakulima waliyotayarisha vyakula hivyo, au kulima mazao kwenye mashamba yao katika vijiji mbalimbali nchini.

Pia Soma

Advertisement
Mkurugenzi mkazi msaidizi wa WFP,  Wendy Bigham amesema wachuuzi wanaouza kwenye soko hilo ni makundi ya wakulima wadogo ambao hawapo kwenye sekta ya biashara.

Amesema baadhi ya vyakula vinavyopatikana kwenye soko hilo ni bidhaa za mkakati kwa ajili ya lishe.

Chanzo: mwananchi.co.tz