Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Soko la Ndugai, stendi mpya rasmi Jumatatu

Soko Kuuuuuuu Ed Soko la Ndugai, stendi mpya rasmi Jumatatu

Fri, 5 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge, ameagiza kuanza kutumika kwa Soko Kuu la Ndugai, kituo cha mabasi na maegesho ya malori ifikapo Juni 8 mwaka huu (Jumatatu) kutokana na kukamilika kwa ujenzi wake.

Alitoa agizo hilo jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini hapa kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa.

Alisema ujenzi wa miradi hiyo umekamilika na kuagiza huduma za usafiri katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani kilichoko Viwanja vya Nanenane kuhamishiwa kwenye kituo kipya.

“Terminals' zote zilizokuwa zinatumika, tunazipa muda wa siku 30 ili nao wahamie stendi mpya na 'terminals' zao zitabaki na kazi ya 'service' za magari yao tu," alisema.

Dk. Mahenge alisema viwanja wa Nanenane vitaendelea kuwa kituo cha daladala, lakini kutakuwa na kituo cha daladala kwenye soko na kituo kipya cha mabasi.

Alisema baada ya kujengwa kituo maalum cha daladala, shughuli za daladala zote zitahamia huko na viwanja vya Nanenane vitabaki kwa ajili ya shughuli za wakulima na wafugaji.

Alisema maegesho ya malori yako eneo la Nala na yana uwezo wa kuegesha malori 300 yenye zaidi ya tani tatu, hivyo ifikapo tarehe hiyo yawe yamehamia kituo hicho.

"Yote hii imeanza baada ya uamuzi wa Rais kuhamishia Makao Makuu Dodoma, na hii miradi ni baadhi tu, ipo miradi mikubwa ambayo utekelezaji wake umeanza ukiwamo ujenzi wa uwanja wa ndege ambao wananchi wamelipwa fidia na fedha zimeshatengwa, lakini uwanja wa zamani umeboreshwa na sasa ndege zinatua hadi usiku," alisema.

Dk. Mahenge pia alisema upo mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara ya mzunguko yenye urefu wa kilometa 110 ambayo mchakato wa ununuzi unakamilishwa ili uanze.Kiongozi alisema anamshukuru Rais Magufuli kwa kulifanya Jiji la Dodoma kuwa la kisasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live