Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skimu mpya 25 za umwagiliaji kujengwa nchini

Wadudu Dawa Kilimo Skimu mpya 25 za umwagiliaji kujengwa nchini

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika mwaka ujao wa fedha wa 2024/2025, Serikali inatarajia kujenga skimu mpya 25 za umwagiliaji katika maeneo mbalimbali nchini ili kuongeza kasi ya uzalishaji katika sekta ya kilimo.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 bungeni jijini Dodoma Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema mbali ya skimu hizo mpya pia watakamilisha ujenzi wa mabwawa 14 yenye mita za ujazo Milioni 131.5 na ukarabati wa skimu 30 zenye jumla ya hekta 41,771.

Aidha, Serikali itakamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa skimu 28 kati ya 42 na mabonde ya kimkakati 17 kati 22 yaliyopangwa mwaka 2022/2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live