Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skimu 384 kujengwa miaka mitano ijayo

Rwanda Irrigation Scheme Skimu 384 kujengwa miaka mitano ijayo

Mon, 22 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TUME ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), inatarajia kujenga na kukarabati skimu 384 zitakazogharimu kiasi cha Sh. bilioni 986.8, ili kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki jijini hapa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Daudi Kaali, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya sekta ya uwagiliaji kwa miaka mitano na mikakati ya miaka mitano ijayo.Alisema skimu hizo zitajengwa kwa miaka mitano ijayo kwenye mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Tabora na Katavi na zitaongeza eneo la umwagiliaji kwa hekta 400,491.8."Fedha hizo zitakazotumika zitatokana na programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) ambapo serikali itachangia asilimia 41 ya gharama hizo sawa na Sh.bilioni 80.9 kwa mwaka," alisema.

Mkurugenzi huyo alisema ujenzi na ukarabati huo wa miundombonu ya umwagiliaji utatumia utaratibu wa 'force account' ili kuondokana na tatizo la ucheleshaji miradi na kupunguza gharama za utekelezaji."Matarajio yetu ni kuhakikisha tija katika uzalishaji kwa mazao mbalimbali katika skimu zote za umwagiliaji nchini inaongezeka," alisema.Kaali alisema hatua hiyo itaongeza mchango wa sekta hiyo katika uhakika wa chakula nchini kutoka asilimia 24 ya sasa hadi asilimia 30 ya mahitaji yote ya chakula ifikapo mwaka 2025.

Pamoja na mikakati hiyo, Mkurugenzi huyo alisema kuna tatizo la uhaba wa fedha za kutekeleza shughuli za umwagiliaji ambapo fedha zinazotengwa ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji halisi na pia wakati mwingine hazitoki kwa wakati.Aidha alisema katika msimu wa mwaka 2019/20, skimu 40 zilipata athari ya mafuriko na kwasasa Tume hiyo inaendelea kufanya tathmini ya uharibifu huo ili kujua gharama za ukarabati wake."Pia Tume inakabiliwa na uhaba wa wataalam wa umwagiliaji ambapo kuna watumishi 213 kati ya 438 wanaohitajika na hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 225,"alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live