Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida yapata ziada mazao ya chakula

C95b8c0d21ff6f2c2ad8cf672db20075 Zao la alizeti hustawi mkoani humo

Sun, 10 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkoa wa Singida umejipatia ziada ya tani 377,192.8 za mazao mbalimbali ya chakula sawa na asilimia 178.5 katika msimu wa kilimo 2020/2021 na 2021/2022.

Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu Mkoa wa Singida, Beatrice Mwinuka alieleza hayo wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri mkoa (RCC) mjini hapa.

Alisema kuwa mkoa umepata mafanikio hayo baada ya kuzalisha jumla ya tani 821,881.7 za mazao hayo zilizolimwa sehemu mbalimbali za mkoa.

Aidha, alisema tani 286,350.7 za alizeti na pamba zilivunwa ikiwa ni kiasi kidogo ikilinganishwa na mavuno ya mazao ya chakula kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Wakati huo huo, Mwinuka alisema kuwa msimu huu mkoa unatarajia kuvuna tani 1,166,464.7.

"Kiasi kilicholengwa kuzalishwa kitauhakikishia mkoa usalama na upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake wote kwa mwaka mzima. Kwa mazao ya kimkakati ya alizeti, korosho, mkonge na pamba mkoa utazingatia kanuni za kilimo ili kufanikisha shughuli hiyo," alisema.

Awali, akifungua kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Binilith Mahenge aliwataka wajumbe kwenda kusimamia vizuri yale yote yanayoamuliwa kwa manufaa mapana ya maendeleo ya mkoa.

Aliwaagiza viongozi wa ngazi mbalimbali kuendelea kuelimisha na kuhimiza wananchi kushiriki ipasavyo shughuli za uwekaji anuani za makazi na sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live