Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simu za mkononi zatajwa kuwa msaada kwa wanawake kiuchumi

Fri, 14 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Matumizi mazuri ya simu za mkononi miongoni mwa wanawake si tu yatawasaidia kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidunia bali yametajwa kusaidia kaya masikini kuinua kipato, utafiti umebaini.

Utafiti mpya uliofanywa na Taasisi ya Repoa umebaini kuwa, asilimia 70 ya wanawake kwenye kaya masikini waliweza kutumia simu kwaajili ya shughuli za maendeleo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti huo ulioitwa ‘Umiliki na Matumizi ya Simu miongoni mwa Wanawake’, leo Alhamisi Desemba 13, 2018 Mkurugenzi wa Repoa,Dk Donald Mmari amesema kaya masikini zinaweza kusaidiwa kwa kumwezesha mwanamke kutumia teknolojia ya simu katika shughuli zake.

"Katika miaka ya karibuni kumekuwa na mabadiliko makubwa na ubunifu katika kutoa huduma za kifedha."

"Tumeangalia ni jinsi gani akina mama ambao wameshindwa kuzimiliki simu na wakapata mafunzo ya namna yakuzitumia huduma za kifedha ili kuleta mabadiliko ya maisha hasa kupata kipato," amesema.

Utafiti huo ulifanyika kati ya Julai 2016 hadi Novemba 2017 ulihusisha wanawake 2,000 kutoka mikoa  ya Arusha, Iringa,Mwanza, Tanga na Ruvuma ukizingatia kaya masikini ili kuona jinsi matumizi ya huduma za kibenki (Simu-bank) zinavyoweza kuchochea maendeleo.

Mtafiti Mwandamizi, Dk Flora Myamba amesema simu imeleta matokeo chanya kwa wanawake kuwasaidia kuzifikia fursa mbalimbali za maendeleo.

Dk Myamba amesema asilimia 70 ya wanawake hao walizitumia simu kwa ajili ya shughuli za kiuchumi ikiwamo kununua pembejeo, kuanzisha biashara pamoja na kufuatilia taarifa za masoko ya bidhaa.

"Wanawake wengi wameweza kuzitumia simu kwa shughuli za kujiongezea kipato," amesema.

Hatahivyo, utafiti huo umebaini kuwa asilimia 30 ya wanawake kutoka kwenye kaya hizo walipoteza simu kutokana na sababu mbalimbali.



Chanzo: mwananchi.co.tz