Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simu za Mkononi: Mbadala wa masanduku ya Posta

Simu Janjaaa Shirika la Posta nchini limezindua huduma za kidijiti

Fri, 6 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huenda huduma za kupokea na kutuma barua na vifurushi zikamfikia kila mtumiaji wa simu Tanzania, baada ya huduma za posta kuunganishwa na mtandao wa simu nchini.

Shirika Posta Tanzania (TPC) limesema kukamilika kwa usajili wa makazi kunaenda sambamba na uboreshaji wa anuani za masunduku ya posta ambapo namba za simu zitatumika kama mbadala wa anuani hizo.

Meneja wa TPC Mkoa wa Mwanza na Geita, Dongwe James akizungumza leo Mei 5, 2022 jijini Mwanza, amesema maboresho hayo yatarahisisha shughuli za maendeleo na kuimarisha ulinzi na usalama wa Taifa.

"Zamani watumiaji wa posta walikuwa wanaandika anuani ya posta pekee, hivi sasa tumeboresha kuendana na mabadiliko ya teknolojia, mteja anapotuma bahasha yake posta ataandika anuani yake, namba ya nyumba anayoishi na simu yake ya mkononi na mzigo wake atafikishiwa mpaka mlangoni,” amesema Dongwe. Amesema anuani za makazi na ukuaji wa teknolojia ni muhimu kwa usalama wa Taifa na watumiaji wa huduma za posta kote duniani.

Meneja huyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa watendaji wanaotekeleza suala hilo ili kwenda sambamba na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha zoezi la anuani na makazi.

Wakizungumza na Nukta habari baadhi ya wakazi jijini Mwanza wamepongeza jitihada zinazofanywa na shirika hilo na kwamba zitasaidia katika kurahisisha utoaji wa huduma.

Abel Nkurumba, mkazi wa jijini hapa amesema zaman walipopeleka mzigo au barua walilazimika kusubiri miezi au wiki ndipo mzigo ufike lakini hivi sasa ndani ya masaa 24 au 48 unapata mzigo wako.

"Huduma zimerahisishwa ni tofauti na zamani na hii ya anuani za makazi itaongeza urahisi wa mzigo au kifurushi kufika bila kupotea,” amesema Nkurumba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live