Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simu 1.6 milioni zilifungiwa na TCRA mwaka 2018

37305 TCRAPIC Simu 1.6 milioni zilifungiwa na TCRA mwaka 2018

Sun, 20 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Zaidi ya Simu za mkononi 1,677,750 zilizobainika kutofikia viwango, kupotea na kuibiwa zilifungiwa huduma na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) hadi kufikia Desemba 2018.

Hayo yamesemwa na Rais John Magufuli leo Ijumaa Januari 18, 2019 katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS) iliyofanyika ofisi za TCRA jijini Dar es Salaam.

Amesema mfumo huo umekuwa na uwezo wa kufahamu idadi ya vifaa vinavyounganishwa kwa huduma ya mtandao nchini ambavyo vimefika 27.9 milioni, taarifa za laini ya simu na namba tambulishi ya vifaa vya mawasiliano.

“Lakini pia imetusaidia kujua miamala ya kifedha inayofanyika kwa njia ya mitandao ambapo tumesikia kuwa mwaka jana miamala yenye thamani ya Sh139.2 trilioni ambayo ni sawa na wastani wa Sh11.6 trilioni kwa mwezi ilifanyika,”

“Hii ni kielelezo kuwa Serikali iko tayari kushirikiana na sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,” amesema Rais Magufuli.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz