Dar es Salaam. Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye ametangaza kujiuzulu kuanzia Machi 31, 2020 baada ya kuitumikia taasisi hiyo kwa miaka nane.
SOMA ZAIDI: VIDEO: Simbeye aeleza alivyomshawishi Mufuruki kuwa mwenyekiti TPSF
Jana Ijumaa Februari 7, 2020 kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi, kaimu mwenyekiti wa taasisi hiyo Angelina Ngalula alitoa taarifa ya kujiuzulu kwa Simbeye.
“Kwa niaba ya bodi ya wakurugenzi napenda kuwataarifu wanachama wa TPSF, wabia, wadau na umma kwa ujumla juu ya kujiuzulu kwa Simbeye..., Simbeye alikuwa na mchango mkubwa sana kwa taasisi yetu tangu alipojiunga nayo,” anaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Ngalula amesema Simbeye aliyehudumu nafasi hiyo tangu mwaka 2012 amejiuzulu ili apate muda wa kutekeleza majukumu yake mengine.
SOMA ZAIDI: TPSF yataka sera ya vijana kuanzisha biashara bila masharti ya benki
Pia Soma
- Trump atimua wawili waliotoa ushahidi dhidi yake
- Magufuli atunuku kamisheni kwa askari 128
- AFYA: Ndizi mbivu sio nzuri kwa kila mtu
TPSF imewahakikishia wanachama, Serikali, wadau wa maendeleo na sekta binafsi kwa ujumla kwamba itahakikisha hakuna athari zitakazotokea katika kipindi hicho cha mpito wakati wakitafuta mtu mwingine wa kuchukua nafasi hiyo.
SOMA ZAIDI:Sekta binafsi yamlilia bilionea Ali Mufuruki