Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Silinde atinga bandarini uhaba wa Sukari...

Hii Hapa Bei Elekezi Ya Sukari Silinde atinga bandarini uhaba wa Sukari...

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amewatoa hofu Wananchi kuhusiana na Suala la Uhaba wa Sukari, akisema kuwa Serikali iko makini kuhakikisha Bidhaa hiyo inaendelea kupatikana kwa Wingi kwenye mikoa yote nchini na wakati wowote.

Naibu Waziri Silinde ametoa hakikisho hilo, alipofanya ziara Bandari ya Dar es Salaam na kushuhudia Tani 25000 ya Sukari Ikishushwa na kupelekwa kwa Mawakala wakubwa kwa ajili ya Kusambazwa kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Akiwa hapo Naibu Waziri Silinde amesema Sukari iliyopo nchini inatosha kwa mahitaji ya Siku 20 na kuongeza kuwa ndani ya siku 5 Jumla ya tani 27000 ya Sukari ilishushwa katika Bandari ya Dar es Salaam, ambapo imeshaanza kusambazwa mikoani kupitia mawakala wakubwa.

Katika hatua nyingine Naibu waziri Silinde amewataka Wafanyabiashara wa Sukari kuuza Bidhaa hiyo kulingana na Bei Elekezi ambao watakaidi watakumbana na mkono Sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live