Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Silaa: Serikali ikamilishe haraka tafiti vinasaba kwneye mafuta

Mafuta Ya Petrol Silaa: Serikali ikamilishe haraka tafiti vinasaba kwneye mafuta

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Umma (PIC) kwa kipindi cha kuanzia Februari 2022 hadi Januari, 2023, Jerry Silaa (Mb), amesema Shirika la Viwango Tanzania lilipewa jukumu la kuweka vinasaba kwenye mafuta mwaka 2021 kutokana na malalamiko ya wafanya biashara ya kulipa gharama kubwa kwa mzabuni kwa huduma hii ya kuwekewa vinasaba jambo ambalo si la kutozwa gharama kubwa.

Na kwa kuwa vinasaba hivyo vinavyowekwa kwenye mafuta vilikuwa vinaagizwa kutoka nje wakati wa mzabuni na sasa Shirika la Viwango bado linaendelea kuagiza vinasaba hivyo kutoka nje na kuongeza gharama za uendeshaji, na kwa kuwa kuongezeka kwa gharama hizo ni moja ya sababu zinazopelekea uhaba wa fedha za kutekeleza shughuli za TBS ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo kikamilifu.

Kwa hiyo Bunge linaazimia kwamba, TBS wakamilishe kwa haraka tafiti wanayoifanya ya vinasaba vyao wenyewe na kuanza kutumika kwa vinasaba, ili kuondokana na kadhia ya kuagiza vinasaba kutoka nje. Hatua hii itasaidia kuthibiti ubora wa mafuta zaidi na kulinda mapato ya Serikali ipasavyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live