Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sifa za jengo la ghorofa 70 litakalojengwa Zanzibar

Zanzibar Pic Jengo la ghorofa 70 litakalojengwa Zanzibar

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: Africa Press

Zanzibar itaingia kwenye historia itakapokamilisha ujenzi wa jengo la ghorofa 70 ambalo litakuwa na huduma mbalimbali.

Jengo hilo litakuwa la kwanza Afrika Mashariki na kati litajengwa katika kisiwa cha Chapwani Mjini Unguja ambapo litahusisha hoteli na maeneo mengine ya biashara.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kukamilika kwa makubaliano ya baina ya kampuni ya Kitanzania AICL Group na kampuni ya XCassia yenye utaalamu na uzoefu wa kusanifu na kuchora ramani za majengo marefu duniani kupitia uongozi wa Edinburg Crowland Management Ltd yenye ofisi zake katika majiji ya New York na Dubai.

Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo wa AICL Group, Emmanuel Umoh amesema hoteli hiyo itakuwa na maeneo mengine ya kwa ajili ya biashara.

"Ujenzi wa hoteli hii utafanyika kwa awamu tofauti na unatarajia kukamilika baada ya miaka minne," amesema

Amesema jumla ya dola za Marekani 1.3 bilioni zimetengwa kwa ajili ya hatua za awali.

Hizi ni sifa za jengo hilo.

1. Ujenzi utagharimu $1.3 bilioni (TZS trilioni 3.01)

2. Litakuwa jengo la pili kwa urefu Afrika (mita 385, ghorofa 70)

3. Litatumia eneo la mita za mraba 370,000

4. Sehemu kubwa ya mchanga (tani 35,000) kwa ajili ya ujenzi utatoka bara.

Mkurugenzi Mkuu na msanifu wa kampuni ya XCassia Jean-Paul Cassia amesema mradi huo ulitakiwa kuanza miaka mingi iliyopita lakini ulikwama kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vikao, majadiliano, kukubali na kutokubaliana, tafiti za mazingira na kukosekana kwa mtu sahihi wa kuwekeza.

Pia alitaja changamoto za urefu wa jengo hilo litakalo kuwa na urefu wa mita 385, bahari na upatikanaji wa miundombinu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga amesema hatua hiyo ni Mapinduzi makubwa visiwani humo huko akionya watakaobainika kufanya urasimu wakati wa Utekelezaji mradi huo watachukuliwa hatua.

Jengo hilo litakaloitwa Zanzibar Domino Commercial Tower itajengwa umbali wa kilometa 15 kutoka Mji Mkongwe katika eneo la hekta 20 ikiwa na ukumbi mkubwa wa mikutano utakaobeba watu 1,000.

Chanzo: Africa Press