Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shughuli za uchimbaji madini zaimarika Tanzania

Madyyy Kampuni za madini 961 za kizalendo zimesajiliwa

Sat, 21 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shughuli za utafiti na uchimbaji madini zimeongezeka katika kipindi cha miaka minne iliyopita, jambo lililochangia uanzishwaji miradi mikubwa ya uchimbaji wa madini na ajira hasa kwa vijana.

Pia kumekuwepo na uboreshaji wa njia bora za kufanya uzalishaji, uchenjuaji, usafirishaji, ukataji na usanifu wa madini.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Tanzania, Profesa Idris Kikula akizungumza leo Mei 20, 2022 kwenye ufunguzi wa jukwaa la kwanza la utekelezaji wa ushirikishwaji Watanzania katika sekta ya madini tangu mwaka 2018, amesema yapo mafanikio makubwa yamefikiwa kupitia sekta hiyo ikiwa ni pamoja na fursa za ajira.

Profesa Kikula amesema katika kipindi cha miaka minne iliyopita ajira kwa kwa Watanzania katika migodi mikubwa na ya kati zimeongezeka kutoka 6,668 mwaka 2018 hadi kufikia 14,308 mwaka 2021.

Ongezeko hilo limechangiwa na Watanzania kupewa kipaumbele kwenye ajira zote nchini.

“Mafanikio mengine ni pamoja na ongezeko la kiwango cha manunuzi ya bidhaa na huduma zinazotolewa na Watanzania na kampuni za kitanzania ambapo kiwango hicho katika mwaka 2018 kilikuwa ni jumla ya Dola za Marekani milioni 238.71 (Sh555.2 bilioni) sawa na asilimia 46 ya manunuzi yote, na mwaka 2021 kufikia jumla ya Dola za Marekani bilioni 2.1 (Sh4.8 trilioni) sawa na asilimia 97 ya manunuzi yote,” amesema Profesa Kikula.

Pia kumekuwepo na ongezeko la idadi ya watoa huduma Watanzania na kampuni za kitanzania ambapo zimefikia 961 mwaka 2021 sawa na asilimia 61 ya watoa huduma wote katika kipindi hicho.

Ukuaji wa teknolojia katika sekta ya madini ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa matumizi ya mitambo yenye uwezo mkubwa katika uzalishaji wa madini.

​Awali Kamishna wa Madini, Dk Abdulrahman Mwanga amesisitiza kuwa Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta ya madini kwa wananchi, na kuwataka kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo utoaji huduma kwenye migodi ya madini kama vile vyakula, ulinzi, ajira na uuzaji wa bidhaa mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live