Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shirika la Ndege la Uturuki kubadilishwa jina

Turkish Xian Shirika la ndege la Uturuki kubadilishwa jina

Wed, 15 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema shirika la ndege la Uturuki litabadilisha jina lake na kuwa “Türkiye Hava Yolları” badala ya “Turkish Airlines” kama sehemu ya kushinikiza nchi yake ijulikane kimataifa kama “Türkiye” badala ya ‘Turkey’.

Mapema mwezi huu Nchi hii ilituma barua kwa Umoja wa Mataifa ikisajili rasmi jina la nchi hiyo kama ‘Türkiye’ ikisema jina hili jipya linawakilisha vyema utamaduni na maadili ya Kituruki huku baadhi ya Wachunguzi wa mambo wakisema hatua hii ni sehemu ya juhudi za kulitenganisha jina lake na jina la bata mzinga ambaye ni ‘Turkey’ kwa kiingereza.

“Turkiye haipo tena, sasa ni Türkiye” ambapo maneno ‘Türkiye Hava Yolları’ yataandikwa kwenye ndege zetu zote badala ya Turkish Airlines, “Hava Yolları” inamaanisha mashirika ya ndege kwa Kituruki.

Umoja wa Mataifa na NATO wameanza rasmi kutumia “Türkiye” badala ya “Uturuki.” Baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa kigeni wanaotembelea Ankara pia wamebadilisha jina hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live