Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilingi trilioni 1.1 za kusanywa soko la Dhahabu Geita

Madini Geita Soko la madini ya dhahabu laingiza Shilingi Trilioni 1.1 kwa miaka mitatu

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: mwananchidigital

Kilo 10,780 za madini ya dhahabu zenye thamani ya Sh1.1 trillion zimeuzwa katika soko kuu la dhahabu mjini Geita toka kuanzishwa kwa soko hilo mwaka 2018 hadi Julai 2021.

Pia kilo 3,246 zimeuzwa kwenye masoko madogo ya dhahabu yaliyopo kwenye halmashauri tano zilizopo mkoani hapa.

Hayo yamesemwa leo septemba 22, 2021 na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemery Senyamule wakati wa hafla ya ufunguzi wa maonyesho ya nne ya teknolojia na uwekezaji kwenye sekta ya madini yanayo endelea mkoani Geita.

Senyamule amesema mbali na uzalishaji huo pia mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017 yamewezesha kupatikana kwa zaidi ya Sh 28.2 bilioni kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) katika fedha zinazotokana na uwajibikaji wa makampuni kwa jamii ambazo zimewezesha mabadiliko makubwa katika miundo mbinu ya afya na elimu.

Amesema pamoja na mafanikio yanayopatikana katika sekta ya madini lakini ipo changamoto kubwa ya uharibifu wa miundo mbinu unaofanywa na wachimbaji wadogo kwa kukata miti kwa ajili ya kutengeneza matimba.

Amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo mkoa kwa kushirikiana na wadau wameanza kutoa elimu ya kutumia teknolojia ya vyuma ili kuokoa mazingira.

Akizungumzia maonyesho hayo ambayo kwa mwaka huu ni ya nne, amesema kumekua na ongezeko la washiriki kutoka washiriki 338 hadi 481 ambapo kwa mwaka huu yamehudhuriwa pia na nchi nyingine kutoka Rwanda, Dubai, Congo, India na Uganda.

Chanzo: mwananchidigital