Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema Serikali inaiangalia sekta binafsi kwa mtazamo chanya wa kuwa mdau muhimu wa uchumi na maendeleo.
Dkt. Mwinyi amesema hayo alipofungua mkutano mkuu wa 15 wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar.
Ameesema kazi ya kuandaa sheria inayohusisha maendeleo ya sekta binafsi inaendelea chini ya wizara ya Viwanda na Biashara ikisimamiwa na Sekretarieti ya Baraza la Taifa la Biashara.
Rais Mwinyi amemtaka waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibr, Omar Ramadhan Shaaban kusimamia kukamilika kwa sheria hiyo mwishoni mwaka huu.