Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shehena ya mahindi yazuiliwa mpaka wa Holili

Mahindi Shehena ya mahindi yazuiliwa mpaka wa Holili

Fri, 2 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara wa mahindi katika soko la Kimataifa la mazao Holili, Mkoani Kilimanjaro leo Juni Mosi wameandamana mpaka ofisi za Forodha mpakani mwa Kenya na Tanzania, baada ya shehena za mahindi kuzuiwa katika mpaka huo kuingia Kenya.

Wafanyabiashara hao wameeleza kukwama katika mpaka huo kwa siku nne baada ya kuzuiliwa kupeleka mahindi nchi jirani hali ambayo imezua sintofahamu kwa wafanyabiashara hao.

Mwananchi limefika katika eneo hilo na kushuhudia shehena hizo za mahindi zikiwa kwenye foleni ambapo muda mfupi baadaye magari hayo yaliruhusiwa kuendelea na safari.

Kufuatia hali hiyo, Gazeti hili lilimtafuta Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, James Jilala kujua ni kwanini magari hayo yenye shehena hiyo yamezuiliwa ambapo amesema wao wamepata maelekezo kutoka juu kusitisha mahindi kutokutoka nje ya mpaka huo.

"Tulipata taarifa kutoka kwa viongozi wa juu kwamba tusitishe mahindi yasitoke nje ya nchi ya Tanzania na baadaye tumeletewa taarifa hilo zoezi limeahirishwa kwa muda wa siku kadhaa na wameambiwa ni baada ya muda ndio sasa litakuwa limekuja zuio," amesema Jilala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live