Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shehena ya Uganda kuanza kupitia bandari Dar

Bandari Dar Es Salaam Shehena ya Uganda kuanza kupitia bandari Dar

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) inatarajia kuanza kutoa huduma ya kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kupitia reli ya kati kwenda Mwanza hadi Bandari ya Port Bell nchini Uganda Desemba, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa jijini Mwanza na Mkurugenzi

wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Freddy Liundi kwenye kikao baina ya wadau wa usafirishaji nchini pamoja na wale wa nchini Uganda kuona namna ya kufanikisha kazi hiyo.

Alisema baada ya kukamilika kwa kazi ya kufanyia maboresho miundombinu ya reli na meli, wadau wa usafirishaji wa mizigo kutoka nchini Uganda wameonesha nia ya kutaka kutumia usafiri wa hapa nchini katika kufikisha mizigo yao nchini

Uganda badala ya kupitia Bandari ya Mombasa.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel alisema hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuitumia ili kujiongezea kipato chao na taifa kwa ujumla na hivyo kuwezesha kuchochea maendeleo ya nchi.

“Baada ya kuanza kwa kazi kubwa za kurekebisha miundombinu ya reli ya kati na kwenye bandari ni faraja kuona sasa hadi

nchi nyingine zimevutiwa kutaka kutumia eneo la nchi yetu kwa ajili ya kazi hiyo,” alisema.

Gabriel alisema kwamba sasa Kampuni ya Huduma ya Meli (MSCL), TPA na reli zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya maboresho ya miundombinu yake na hivyo kuwa na ufanisi mkubwa wa utendaji kazi.

Meneja Masoko na Biashara wa MSCL Mwanza, Anselm Namala alisema sasa wana MV Wimbi

ambayo ina uwezo wa kubeba tani 120 na wanatarajia pia kuitumia MV Umoja ambayo nayo ina uwezo wa kubeba tani 400 za shehena kutumika katika ubebaji wa mizigo.

Alisema eneo la bandari ya Mwanza lina uwezo mkubwa wa kupokea mizigo na kuhifadhiwa vizuri bila kuharibika na vilevile juhudi zinaendelea kuchukuliwa za kutengeneza meli nyingine ya kubeba mizigo ili kutoshe-

leza mahitaji.

Mkuu wa kitengo cha utendaji wa Shirika la Reli Uganda (URC), Ochaki Abubakar alisema wanafurahi kuona sasa wanarejea tena kuanza kupitishia mizigo yao Tanzania baada ya kusitishwa mwaka 2019.

Alisema Uganda inaona usafirishaji wa mizigo yao kupitia reli ya kati hadi nchini kwao kama eneo sahihi kwa mahitaji yao kuweza kuwafikia kwa wepesi zaidi na kwa gharama nafuu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz