Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shehena kubwa ya makaa ya mawe kusafirishwa kutoka Mtwara kupelekwa Ulaya

ETG SOUTHERN CROSS Meli ya mizgo MV. EGT Southern Cross

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meli ya mizgo MV. EGT Southern Cross inatarajia kusafirisha Tani 59960 za Makaa ya Mawe kwenda Amsterdam Uholanzi, hii ikiwa ni shehena kubwa zaidi ya Makaa ya Mawe kusafirishwa Kupitia Bandari ya Mtwara.

Akizungumza jana mjini hapa, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano, Bw. Nicodemus Mushi amesema, usafirishaji wa Shehena hii kubwa kwenda Bara Ulaya ni hatua muhimu ya kulifikia Soko kubwa la Bara la Ulaya baada ya bidhaa hiyo kuwa na Soko la uhakika katika Bara Asia.

Akifafanua zaidi alisema shehena kubwa ya mwisho ilikuwa tani 59815. “Hii ndio Mara ya kwanza kwa shehena kutoka Bandari ya Mtwara kwenda Bara la Ulaya moja kwa moja,” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa Masoko na Uhusiano, Bw. Mushi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti akizungumza alisema, Serikali ya Mkoa wa Mtwara inaridhishwa na utendaji wa TPA na Bandari ya Mtwara hasa katika kutafuta wateja.

Alisema uwekezaji wa Serikali mkoani Mtwara ni mkubwa, ikiwemo Ujenzi wa gati ambao umegharimu Shilingi Bilioni 157.8.

Aidha aliongeza kuwa Serikali imeiwezesha TPA kununua vitendea kazi na kuboresha mazingira ya kufanya kazi hivyo kuna kila sababu ya kuunga mkono jitihada hizi za TPA.

“…Ili kupata Wateja zaidi na sasa Mwelekeo Uwe katika Nchi Jirani ya Comoro ambayo ina fursa kubwa ya kufanya Biashara na Tanzania. Kwa kushirikiana na Kampuni ya Ruvuma Coal tunaendelea kutafuta Masoko zaidi ili kuufanya uwekezaji wa Serikali katika Bandari ya Mtwara kuwa na tija,” alisema Brigedia Jenerali Gaguti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live