Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabaha ya maonyesho ya sabasaba 2019 yabainishwa

65246 Pic+sabasaba

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Dk Ng'wanza Kamata  amesema lengo la maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Tanzania kando kando ya Barabara ya Kilwa  ni kuhakikisha kilimo na viwanda vinabebana.

Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo leo Jumanne Julai 2, 2019, Dk Kamata amesema kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema "usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu' hivyo shabaha yao siyo kuungana na kauli ya kuwa Tanzania ya viwanda pekee bali kuangalia aina ya viwanda vinavyoanzishwa kama vinaendana na matarajio ya uwapo wa viwanda Tanzania.

Amesema jambo lingine ni kuangalia ubora wa bidhaa zinazozalishwa kama zinakidhi viwango vilivyokusudiwa.

Amefafanua shabaha nyingine ni  kuangalia kiasi cha bidhaa kinachozalishwa  kama kinaendana na mahitaji ya biashara.

"Mwitikio ni mkubwa na kila mwaka kukiwa na maonyesho kama haya umekuwa unaongezeka" amesema Dk Kamara.

Dk Kamata amesema nchi za nje zilizoshiriki maonyesho mwaka 2018 zilikuwa 33 mwaka 2019 zipo 35.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz