Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh81 milioni kuneemesha kiuchumi wakazi 2, 884

Pesa Fedhaddd Sh81 milioni kuneemesha kiuchumi wakazi 2, 884

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Wakazi 2,884 katika kata 206 za Mkoa wa Tabora watanufaika na miradi ya kiuchumi ya Sh81 milioni watakayoibuni kupitia kamati za utekelezaji za kata hizo.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Julai 7, 2023 na Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tabora (CCM), Jacqueline Kainja wakati akikabidhi fedha hizo kwa wajumbe wa kamati za utekelezaji za kata za mkoa huo kwenye hafla ya uzinduzi wa miradi hiyo kupitia Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Tabora. Mbunge huyo amesema fedha hizo zitasaidia kuwapa nguvu katika miradi ya kiuchumi watakayoibuni kwenye kata zao na kuwanufaisha wajumbe 2,884 wa kamati za utekelezaji za kata ambao ni 14 kutoka kila kata mkoani humo.

“Tunataka wanufaika hao wawe chachu ya kunufaika ili watakaponufaika basi inufaishe jamii yote inayowazunguka kwenye kata zao na mimi naahidi nitasaidia hata makundi ya vijana wakiwemo bodaboda lakini mkazo utakuwa zaidi kwa wanawake," amesema Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Tabora, Mwanne Mchemba amewapongeza wabunge wa viti maalum mkoani humo, Munde Tambwe na Jacqueline Kainja akidai wanatimiza wajibu wao, kufanyia kazi changamoto na kero zinazowakabiri wapiga kura wao. “Hawa wabunge wa viti maalum wanafanya kazi nzuri na kubwa ukilinganisha na wale wa majimbo; kutolewa kwa fedha hizi na mbunge huyu ni udhibitisho tosha huo ndiyo ukweli hata kama baadhi ya watu watanielewa vibaya nina majimbo 12 lakini wabunge wangu wa viti maalum kiukweli wanafanya kazi nzuri," amesema Naye, Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Dk John Mboya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo, Dk Batilda Burian amesema fedha zilizotolewa zifanye shughuli za kuwainua wananchi kiuchumi katika kata zao huku akisisitiza uwepo wa nidhamu katika matumizi ya fedha hizo kwani zikitumika kama zilivyokusudiwa awamu ijayo zitaongezeka.

Chanzo: Mwananchi