Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh8.4 bilioni kuokolewa mgodi wa Stamigold

97750 Stamico+pic Sh8.4 bilioni kuokolewa mgodi wa Stamigold

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) litaanza kuokoa Sh8.4 bilioni kwa mwaka kwenye mgodi wa Stamigold uliopo Biharamulo mkoani Kagera baada ya kupeleka umeme wa gridi ya taifa.

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Tanesco, Dk Alexander Kyaruzi amesema hayo leo Jumatatu Machi 2, 2020 kuwa mgodi huo unatumia mafuta ghali ya dizeli kuendesha mitambo na baada ya kufikisha umeme wa gridi ya taifa gharama zitatoka Sh1 bilioni hadi Sh300 milioni kwa mwezi.

“Baada ya bodi kutembelea mgodi na kujionea mahitaji ya mgodi na hasara wanayoipata kutokana na kukosa huduma ya umeme nafuu wa Tanesco tutashirikiana na menejimenti kufikisha umeme katika mgodi huu mapema iwezekanavyo kutokea mkoani Geita umbali wa kilomita 90," amesema Dk Kyaruzi

Dk Kyaruzi amesema hayo yote yatatimia baada kukamilika kwa mradi wa umeme wa Bulyahnulu Geita Juni 2020.

Meneja Mkuu wa mgodi wa Stamigold, Gilay Shamika amesema kutokana na kukosa umeme nafuu wa Tanesco, gharama za kiuendeshaji zimekuwa kubwa.

Shamika amesema endapo mgodi utaunganishwa na umeme wa Tanesco, itasaidia kukua kwa mgodi na kuongeza mapato.

Pia Soma

Advertisement
“Hivi sasa tunatumia takribani Sh1 bilioni kuzalisha umeme kwa mwezi lakini kama tukiunganisha na Tanesco tutalipia Sh300 milioni kwa mwezi hivyo tutaokoa takriban Sh8.4 bilioni kwa mwaka ambazo zitaingia kwenye mapato ya Mgodi na Serikali” amesema Shamika

Katika hatua nyingine, Dk Kyaruzi amesema kuanzia sasa mpaka Desemba 2020 mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma itakuwa na umeme wa kutosha baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miradi mikubwa ya kusafirisha umeme wa gridi ya taifa kuanzia Bulyanhulu mpaka Geita, Nyakanazi na wa Nyakanazi mpaka Rusumo.

“Mwekezaji yoyote yule asiwe na wasiwasi kwakuwa tunajenga laini za kusafirisha umeme mkubwa wa msongo wa kilovilti 220 kutoka Bulyanhulu mpaka Geita, tukitoka Geita tunakwenda Nyakanazi na kutoka Nyakanazi tutakwenda Rusumo ambapo tutapata umeme wa megawati 27 pia tutajenga laini nyingine kwenda Kigoma ambapo tutapata umeme wa megawati 45 kutoka kwenye mradi wa bwawa la Malagarasi,” amesema Sk Kyaruzi

Chanzo: mwananchi.co.tz