Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh72 bilioni kuwalipa wakulima wa korosho Tanzania

Thu, 17 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiasi cha Sh72 bilioni zimeshatengwa kwa ajili ya kuwalipa wakulima wa korosho ambao bado wanaidai Serikali ya Tanzania na fedha hizo zitaanza kutolewa na Benki ya Kilimo Jumanne, Oktoba 22, 2019.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Oktoba 16, 2019 na Rais wa Tanzania John Magufuli wilayani Masasi mkoani Mtwara wakati wa ziara yake inayoendelea mkoani Lindi.

Kabla ya kutoa majumuisho hayo, Rais Magufuli alimtaka Naibu Waziri wa Kilimo, Husein Bashe kuzungumzia madeni hayo baada ya wakulima wa korosho ambao bado wanaidai Serikali kulalamikia malipo yao.

“Wakulima wa korosho ambao bado hawajalipwa hapa Masasi wanadai Sh3 bilioni, lakini hawa ni wale ambao akaunti zao zilikuwa na matatizo. Kuanzia Jumanne wiki hii wakulima wote wa Lindi na Mtwara kabla hatujaingia mnada unaoanza mwisho wa mwezi huu watakuwa wamelipwa,” amesema Bashe.

Katika kujiridhisha Rais Magufuli alimuita Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo ambaye alikuwa ameambatana naye kwenye msafara huo na akimtaka kutoa uhakika wa malipo hayo, “Mheshimiwa Rais fedha hizo zipo. Tuna zaidi ya Sh260 bilioni na deni ni Sh72 bilioni na hapa Masasi ninadaiwa Sh3.4 bilioni na zote kuanzia Jumanne tutazimaliza,” amesema mkurugenzi huyo.

Wakati huohuo, Bashe ametumia fursa hiyo kuelezea utaratibu mpya wa uuzaji korosho unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Pia Soma

Advertisement
“Msimu huu utaratibu wa kuuza korosho utakuwa wa wazi hautokuwa wa zamani, wanunuzi watakuja katika vyama vya ushirika wataweka bei zao na mtamjua aliyeweka bei ya juu na mtafanya maamuzi.”

“Mwakani, mfumo utakaotumika wanunuzi wote duniani wataanza kuonyesha bei wanazotaka kununulia na ninyi mtafanya maamuzi hayo ni maelekezo ya serikali.”

“Mtendaji wa bodi wakati tunaendelea na utaratibu huu wiki ijayo mtangaze kwenye magazeti kila eneo ambalo wanunuzi wanatakiwa kwenda kushindanishwa kupitia magazeti yote ya Serikali yatangaze wanunuzi na wakulima wote mfahamu wapi korosho zitashiriki,” amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz