Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh583 milioni kukuza kilimo cha mahindi Njombe

Mahindi Shambani Marufuku Sh583 milioni kukuza kilimo cha mahindi Njombe

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

New Content Item (1) Njombe. Chama cha msingi cha wakulima wa mahindi Ibumila (Amcos) wamepatiwa Sh583 milioni ili kuwasaidia kukuza na kuongeza thamani ya kilimo hicho.

Akizungumza Novemba 11 na wanachama wa Ibumila Amcos, mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la USADF, Gilliard Nkini amesema shirika hilo limeamua kuingia mkataba na wakulima hao ili kuwasaidia namna bora ya kuboresha kilimo hicho cha mahindi na kuwa cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao.

Amesema pamoja na kiasi hicho cha fedha watafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha wanawatafutia masoko ya uhakika ili kuongeza thamani ya zao la mahindi.

"Pia tutawaongezea pikipiki na gari la kuwasaidia kuchukua mahindi na kusambaza ule unga madukani na maeneo mengine," amesema Nkini.

Amesema hiyo itawasaidia wakulima hao kupunguza gharama za kukopa benki hasa ukizingatia kuwa wamekuwa wakisikia kuwa riba ni kubwa.

Kwa upande wake Meneja mradi kutoka USADF, Irene Mwakisese amesema wameamua kuingia mkataba na chama hicho cha ushirika ili kuongeza uzalishaji wa zao la mahindi wilayani Njombe.

"Huu mkataba utawasaidia wana Ibumila kujenga ghala lenye uwezo wa kuhifadhi nafaka tani 1500," amesema Mwakisese.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Christopher Sanga kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amelipongeza shirika hilo kwa kutoa fedha hizo ambazo zitasaidia kuongeza thamani ya zao la mahindi mkoani Njombe.

"Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa chama hicho cha ushirika Ibumila AMCOS ili wakulima waweze kuongeza kipato," amesema Sanga.

Mkulima kutoka chama hicho, Daina Mangula amesema ujio wa mradi huo utasaidia kupunguza changamoto za wakulima ikiwemo utatuzi wa changamoto ya soko la mahindi.

"Tunafurahi sana kupata mkataba huu kwani wa kwanza tumejitahidi kufuata vigezo vyote ili kuona tunakidhi na tuweze kufanikiwa na kwa mafanikio hayo ndiyo maana tumeingia hii awamu ya pili," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live