Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh3 trilioni kujenga viwanda 202 Pwani

Fedhapic Sh3 trilioni kujenga viwanda 202 Pwani

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mradi wa kongani ya kisasa ya viwanda unaojenga viwanda 202 katika eneo la ukubwa wa ekari 1,077 umefikia asilimia 93 katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa miundombinu na utakamilika Februari 2024.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea eneo la mradi huo la Disunyara na Kikongo, wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kujionea utekelezaji unavyoendelea.

Amesema Tanzania iliamua isiachwe nyuma katika mapinduzi ya nne na kuelekeza nguvu katika maendeleo ya viwanda ili kujenga nchi katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa inayoishia mwaka 2025 ambayo imeelekeza kuwe na viwanda.

“Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa utayari wake ulioonesha kuwa ujenzi wa uchumi wa nchi upo mikononi mwa sekta binafsi,” amesema Dkt. Kijaji na kuongeza kuwa mwekezaji wa mradi huo ni KAMAKA Company Limited ya Dar es Salaam anashirikiana na Serikali ya Tanzania.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ameeleza kuwa barabara ya kuanzia Makofia -Mlandizi -Mzenga -Vikumburu - Mloka ni muhimu kwani inapitia eneo la uwekezaji na miradi ya kimkakati na kuomba ujenzi huo ukianza uanzie Mlandizi kwa maslahi mapana ya eneo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live