Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh18 bilioni kutumika ‘kutandika mkeka’ Manispaa ya Ilemela

8811 Pic+mkeka TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Wakazi wa mitaa minane katika Manispaa ya Ilemela wanaokabiliwa na kero ya usafiri kutokana na ubovu wa barabara, sasa wana sababu ya kufurahi baada ya Serikali kutenga zaidi ya Sh18 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.

Mitaa hiyo ni Sabasaba, Kiseke, Buswelu, Isamilo Big Bite, Mji Mwema, Makongoro Junction, Mwaloni na Kigoto.

Akizungumza wakati wa kutia saini mkataba wa ujenzi wa barabara hizo zenye urefu wa kilomita 12.1, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, John Wanga alisema ujenzi utaanza Juni 15 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 15.

Licha ya kujenga barabara, Wanga alisema sehemu ya fedha hizo zitatumika kuweka taa za kuongozea magari na vifaa maalumu vya kuhifadhia taka ngumu kabla ya kuzolewa kupelekwa dampo.

Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga alisema halmashauri imetumia zaidi ya Sh436 milioni kulipa fidia kwa wananchi ambao maeneo na mali zao zimeingia ndani ya eneo la mradi. Fedha hizo ni kati ya Sh636 milioni zitakazolipwa fidia.

Naye mwakilishi wa Kampuni ya Sinohydro Corporation LTD, Jin Bin inayojenga barabara hizo aliahidi utekelezaji wa mradi huo utafanyika kwa viwango na wakati uliokubaliwa kwenye mkataba.

Chanzo: mwananchi.co.tz