Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh1 bilioni kuboresha soko Manzese

Fedhaa 0 Sh1 bilioni kuboresha soko Manzese

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIASI cha Sh bilioni 1.3 zimetengwa na Manispaa ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uboreshaji wa soko la Manzese maarufu soko la kuku.

Ofisa Mfawidhi sehemu ya biashara na masoko katika manispaa hiyo, Geofrey Mbwama amesema fedha hizo zimetengwa kutoka mapato yake ya ndani.

Amesema katika uboreshaji huo manispaa hiyo imepanga kujenga fremu za kisasa kwenye ghorofa ya sakafu tatu ambapo jumla ya fremu 39 zitajengwa.

Amesema manispaa imedhamiria kujenga fremu za kisasa kwa wafanyabiashara wa soko hilo hususani wauza kuku ili kuwawezesha kufanya biashara zao kwenye maeneo rafiki yatakayovutia wateja wao na hivyo kukuza vipato vyao.

Mbwama ametoa rai kwa wafanyabiashara hao kuanza kufanya biashara zao kisasa hususani wafanyabiashara wa kuku ambapo miundombinu itakayokuwepo itawalazimu kutunza kuku kwenye majokofu baada ya kuchinja.

Soko la Manzese Lina jumla ya wafanyabiashara 496 ambapo kati ya hao wafanyabiashara wanaouza kuku ni zaidi ya 100 huku wanaobaki wanajishughulisha na biashara za mama lishe na biashara mchanganyiko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live