Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh bil. 10 zatengwa ukarabati soko Kariakoo

692e8794e941395eb88661a9a841e269 Bashungwa akiwasilisha bajeti ya TAMISEMI

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Masoko ya Kariakoo katika mwaka wa fedha 2022/23, limetengewa kiasi cha Sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa soko hilo kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo Aprili 14, 2022 bungeni Dodoma na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo.

Amesema mradi huo una sehemu kuu mbili, ambapo sehemu ya kwanza ni ukarabati wa soko lililoungua na sehemu ya pili ni ujenzi wa soko la ghorofa sita za juu na ghorofa mbili za chini katika eneo lilipokuwa soko dogo, ambalo limebomolewa.

“Shirika litaendelea kusimamia maeneo mengine ya shirika yaliyopo Tabata Bima, Mbezi Beach Makonde na kuweka mikakati na mifumo thabiti ya uendeshaji wa biashara,” amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live