Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh Bil. 776 kunogesha barabara nchini

D07bf7e3c3f0d597413ac41fbc187988 Sh Bil. 776 kunogesha barabara nchini

Sun, 14 Aug 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amesema mwaka wa fedha 2022/23, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami utakua na urefu wa Kilometa 422.

Pia amesema kiwango cha changarawe urefu wa Kilometa 11,074, madaraja 269 na matengenezo kwa barabara yatakayofanyika ni ya urefu wa Kilometa 21,595.

Ameyasema hayo leo Agosti 14, 2022 katika hafla ya utiaji saini mikataba kati ya TARURA na wakandarasi watakaotengeneza kazi za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/23, ambayo mgeni rasmi alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Bashungwa amesema bajeti ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara vijijini na mijini imeongezeka kutoka Sh bilioni 272.56 mwaka 2020/21 hadi Sh bilioni 722 katika mwaka wa fedha 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 185.

Amesema mwaka wa fedha 2022/23 ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati, ambapo TARURA imetengewa bajeti ya jumla ya Shilingi bilioni 838.16, ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni 776.63 ni fedha za ndani na Sh bilioni 61.53 ni fedha za nje.

Bashungwa amesema mpaka sasa miradi iliyo tayari kusainiwa ni mikataba 968, yenye thamani ya Shilingi bilioni 248.74, na miradi yenye thamani ya Shilingi bilioni 129.83, imetangazwa upya baada ya wakandarasi walioomba kutokidhi vigezo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz