Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serkali yataja mikakati Sita kukabili ongezeko bei ya Pembejeo

David Silinde Naibu (600 X 372) Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwananchi

Serikali imetaja mikakati sita ya kukabiliana na ongezeko la pembejeo ikiwemo kuainisha na kutangaza bei elekezi za mbegu bora kila mwaka ili kudhibiti upandaji holela wa bei za mbegu.

Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde amesema hayo leo Juni 21, 2024 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Stella Fiyao.

Stella amehoji Serikali imejipanga vipi kukabiliana na ongezeko la bei ya pembejeo za kilimo.

Akijibu swa hilo, Silinde amesema mikakati hiyo ni kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima wa mazao yote nchini ili kuwapa unafuu wa bei ya mbolea, kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani.

Chanzo: Mwananchi