Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yazuia vibali kuagiza sukari nje

Sugari Serikali haitotoa Kibali cha kuagiza Sukari.

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema kuwa itasimamia sheria na taratibu iliyojiwekea kwenye usimamizi wa mazao mbalimbali ikiwemo miwa, hivyo haitatoa kibali kwa wafanyabiashara wa sukari badala yake kibali kitatolewa kwa wazalishaji wa ndani kama kutakuwa na uhitaji.

Imebainisha kuwa kwa sasa nchini kuna ziada ya Tani Zaidi ya 70,000 za sukari hivyo serikali haiwezi kutoa kibali chochote cha uagizaji wa sukari nje ya nchi wakati uzalishaji unaendelea nchini.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ametoa kauli hiyo ya serikali mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi na wazalishaji wakubwa wa sukari hapa nchini kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maarufu “Kilimo IV” Jijini Dodoma.

Amesema kuwa serikali kuendelea kutoa kibali kuagiza sukari nje ya nchi sio sahihi kwani inahatarisha uzalishaji wa sukari nchini jambo linalowakosesha ajira watanzania wengi huku likiwakosesha soko la miwa kwa wakulima ambao miwa yao huchomwa kutokana na uwezo mdogo wa viwanda vya ndani.

“Ninawaomba sana wafanyabiashara wote nchini watambue kuwa serikali inapenda sana wapate faida kwenye biashara ya zao hilo lakini hii ya sukari waache tupambane ili tuweze kuzalisha ndani ya nchi” Amekaririwa Waziri Mkenda

Kauli hiyo ya Waziri wa Kilimo inajili wakati ambapo imebainika kuwa kumekuwa na barua nyingi zinazowasilishwa Bodi ya Sukari kwa ajili ya maombi ya kibali cha kuagiza sukari nje ya nchi.

“Mimi ndio msimamizi wa sheria kwahiyo msimuhangaishe sana Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania kwamba yeye anakataa kuwapa ruhusa ya kuingiza sukari, sheria haimruhusu na wala hainiruhusu mimi kutoa kibali hicho” Mhe Mkenda

Chanzo: www.tanzaniaweb.live