Kutokana na kupanda kwa bei ya chakula kulikosababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali imepeleka chakula kwa halmashauri 41 kuwauzia mwananchi mmoja mmoja kwa bei rahisi.
Kutokana na kupanda kwa bei ya chakula kulikosababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali imepeleka chakula kwa halmashauri 41 kuwauzia mwananchi mmoja mmoja kwa bei rahisi. Bashe aliyasema hayo leo, Novemba 22, 2022 alipohutubia wananchi wa Wilaya ya Kondoa wakati wa safari ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenda mkoani Manyara kwa ziara ya kikazo.