Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yazindua mradi wa BBT-Life awamu ya pili

Meli  Uvuviii.png Serikali yazindua mradi wa BBT-Life awamu ya pili

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu imezindua awamu ya pili ya program ya Jenga kesho iliyo bora kwa wanawake na vijana kwa upande wa sekta ya Uvuvi maarufu kama “BBT-LIFE” tukio lililofanyika leo februari 23, 2024 kwenye Wakala ya Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kampasi ya Mbegani Bagamoyo mkoani Pwani.

Uzinduzi huo ambao umetanguliwa na mafunzo ya siku 5 ya kubadili fikra kwa vijana na wanawake 300 waliochaguliwa kunufaika na awamu ya pili program hiyo umefanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Bi. Agness Meena ambaye amewasisitiza vijana hao kuhakikisha wanatumia vema mafunzo kwa vitendo watakayopewa kwa muda wa miezi 3 kwenye vituo walivypangiwa baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo ya Nadharia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Bw.Robert Masingiri amebainisha kuwa utekelezaji wa awamu ya pili ya programu ya BBT-LIFE ni sehemu ya utekelezaji wa program ya Taifa ya kukuza ujuzi nchini kupitia kipengele cha mafunzo ya wanagenzi.

Wakizungumza kwa niaba ya wanufaika wenzao wao, Mshiriki kutoka Zanzibar Bi. Samia Othman na mwingine kutoka Kagera Bw. Marius Juvinali wameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kuingia kwenye awamu ya pili ya programu ya BBT-LIFE ambapo wameahidi kuzingatia yale yote watakayoelekezwa wakati wa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live